Rais Museveni amemfuta kazi waziri mkuu wake Amama Mbambazi.
Kwenye taarifa yake Museveni alimshukuru bwana Mbabazi kwa mchango wake kwa nchi ya Uganda ambapo pia alimtangaza mrithi
wake Ruhakana Rugunda ambaye sasa anasubiri kuidhinihswa na bunge.
Bwana Mbabazi alikuwa anatarajiwa na wengi kuwa mpinzani wa Museveni katika uchaguzi ujao.
Rais Museveni ametangaza kuwa amemteua daktari Ruhakaan Rugunda kama waziri mkuu mpya na uteuzi huo ungeanza kutekelezwa mara moja. 

Waziri mkuu anayeondoka Amama Mbabazi alionekana kuwa angemrithi rais Museveni lakini miaka mitatu ambayo amehudumu katika wadhifa huo uhusiana kati yake na Museveni haujakuwa mzuri.
Mapema mwaka huu chama kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema kuwa rais Museveni ambaye amekuwa uongozi kwa muda wa miaka 28 atakuwa mgombea wake wa pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.

Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mmewe ameonewa.

Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.
 VIA: BBC.