Friday, September 19, 2014

HII NDIYO BRN: WANAFUNZI WATUMIA MUDA WA MASOMO KUFYATUA MATOFALI WASHINDWA KUINGIA DARASANI WIKI NZIMA



WAKATI serikali ikiwa katika utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa, hali imeonekana kuwa tofauti katika shule ya sekondari Mwantini iliyopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga baada ya kukutwa na waandishi wa habari wakifyatua matofali ya shule
majira ya saa 5:00 asubuhi  muda ambao wangetakiwa kuwa darasani wakiendelea na vipindi vya masomo.  Wanafunzi hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo wiki nzima bila kuingia darasani huku wakikosa masomo ambayo ni haki yao ya msingi. 
   Katika mahojiano na waandishi wa habari wanafunzi hao walisema  wanasikitishwa na kitendo cha walimu kuwafanyisha kazi hiyo   muda wa masomo wakati wengine wanajiandaa kuanza mitihani ya kidato cha pili na cha nne jambo ambalo linaweza kusababisha kiwango cha taaluma kushuka na kushindwa kufikia malengo ya matokeo makubwa sasa(BIG RESULTS  NOW BRN).
Wanafunzi wakiendelea na kazi ya kuchanganya mchanga kwa ajili ya kazi ya kufyatua matofali.
Kazi ya kufyatua matofali inaendelea ambapo kwa shule nzima uanzia kidato cha kwanza wanatakiwa kufyatua matofali 20,000 ,ambayo watayagawa kwa idadi kwa kila kidato ili kufikia idadi hiyo.
                                                       Mkuu wa shule msaidizi Mwl. Emmanuel  Macha ambaye amevaa Tisheti nyekundu akisimamia zoezi hilo   ,ambapo alisema  kazi hiyo ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na halmashauri hiyo kwa kuandikiwa barua ikiwataka kuanza ufyatuaji wa matofali ambayo yanatarajiwa kutumika  kujenga jengo la maabara ya shule hiyo.


No comments:

Post a Comment