Walimu
wakuu zaidi ya 50 wa shule za msingi za halmashauri ya Wilaya ya Moshi
mkoani Kilimanjaro wamevuliwa
madaraka na kuhamishwa kwenye vituo vyao vya kazi kutokana na kuwatoza fedha wazazi kwa ajili ya kupata vyeti vya kuhitimu elimu hiyo.
Afisa Elimu ya msingi wa halmashauri hiyo, Simon Sheshe, alisema, hatua hiyo inafuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wazazi wa wanafunzi hao ambao wamekuwa wakitozwa Sh. 10,000.
Sheshe aliliambia gazeti hili kuwa, kuanzia mwaka huu wameanza kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wanafunzi wote wanaomaliza elimu ya msingi kupata vyeti vyao baada ya kumaliza mitihani yao ya darasa la saba.
Alionya kuwa, mkuu yeyote wa shule ya msingi atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani kwa kuwa huo ni wizi wa kuaminika na vyeti hutolewa bure na serikali.
Alisema, tatizo lingine la walimu hao ni kufundisha katika vijiji walivyozaliwa na hivyo kushindwa kuongoza au kutoa maamuzi juu ya jambo fulani na kuwaonea aibu kuwachukuliwa hatua za kisheria watu wanaohusika na vitendo viovu kwa hofu ya mtoto wa mjomba, shangazi, mama mdogo au shemeji.
Wiki mbili zilizopita, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Moris Makoi katika kikao cha Baraza la Madiwani alifichua kuwapo kwa walimu wa aina hiyo katika Wilaya ya Moshi Vijijini na kuonya kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.

No comments:
Post a Comment