Watu saba wamehukumiwa kifo baada ya kuwabaka kwa zamu wanawake wanne nje ya mji
mkuu wa Afghanista,kabul mwezi uliopita.Mwathiriwa mmoja ilibidi alazwe hospitalini kufuatia kitendo hicho huku mwengine akidaiwa kuwa mja mzito.
Hukumu hiyo ya kifo ilitolewa kwa kosa la wizi wa mabavu huku hukumu ya miaka kumi na tano ikisimamia ubakaji.
Rais Hamid Karzai aliunga mkono wito wa watu hao kunyongwa hadharani iwapo watapatikana na makosa.
No comments:
Post a Comment