Thursday, October 23, 2014

UHABA WA MADAWATI UNAVYOWATESA WANAFUNZI MANISPAA YA SHINYANGA WALIA KUUMIA MGONGO.

Wanafunzi wa darasa la pili katika  shule ya msingi Mapinduzi iliyopo manispaa  ya Shinyanga wakiwa wamekaa sakafuni kutokana na upungufu wa madawati  katika shule hiyo ambayo  inawanafunzi  837 kuanzia  darasa  la kwanza hadi  la saba huku madawati yaliyopo ni 147 ambapo  wamekuwa wakilalamika kuumia  mgogo na wengine kulazimika kulala darasani maumivu yanapozidi.
Mfanyabiashara wa magari ya  kusafirisha abiria mjini  Shinyanga Giluti Makula akikabidhi msaada  wa madawati 22 kwa mwalimu  mkuu  wa shule ya msingi Mapinduzi A Savera  Rwabuyogo yenye  thamani ya sh milion mbili na elfu sitini,baada ya kuelezwa hivi karibuni alipoalikwa kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali kuwa kuna upungufu wa madawati ndipo aliahidi kuchangia ambapo ametekeleza ahadi yake.
Wanafunzi wakiwa darasani huku wengine wakiamua kulala kutokana na kudai kuumia mgongo kwa kukaa muda mrefu chini na kuinama kuandika ,ambapo pia hali hiyo inasababisha kuwa na mwandiko mbaya.
Wanafunzi wakiwa darasani wakiendelea na masomo.





No comments:

Post a Comment