Tuesday, October 21, 2014

SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LAWAKUMBUKA WATOTO LAFANYA MAMBO MAKUBWA SHINYANGA.

Watoto  wakifanya  mazoezi   katika  uwanja  wa  CCM  Kambarage manispaa  ya  Shinyanga  kabla ya  kuanza  mashindano  ya  mbio za  kuishi  zilizolenga kusaidia kupaza sauti  za mamilioni  ya watoto wanaoishi katika  mazingira magumu ulimwenguni (RACE  FOR  SURVIVAL) ambayo  yalifanyika kitaifa  mkoani  Shinyanga  huku  waandaaji  wakuu  wakiwa  ni  Shirika  la  kimataifa  la  kuhudumia  watoto Save the  children.
Afisa  ulinzi na  usalama  wa  mtoto  kutoa  Save the  children  Shinyanga  Herman  Mbunda akitoa  taarifa yautangulizi wakati wa maadhimisho  ya mbio za kuishi  (RACE FOR SURVIVAL),ambapo alisema  matukio ya  ukatili  kwa  watoto bado ni  changamoto  kubwa  mkoani  humo na kuitaka jamii  kushirikiana  ili  kumaliza  tatizo  hilo.
Mwakilishi wa mkurugenzi wa nchi  ya Tanzania  Jesminka  Milovanovic  amesema lengo  ni  kuhakikisha  kila mtoto anakuwa na uhakika  wa  kupata  huduma zilizobora ikiwa ni  pamoja  na lishe  nzuri , sanjari  na  huduma kutoka  kwa  mtaalamu  wa afya  ambaye atatoa huduma  muhimu  zitakazo muwezesha   mtoto kuwa  na  afya bora.
Watoto  wakifanya  maandalizi  kabla ya kuanza mbio  za kupokezana vijiti
Balozi  wa Save  the children na katibu  mkuu wa shirikisho  la riadhaa  Taifa  Suleiman  Nyambui  akisisitiza  umuhimu wa  michezo ili kuwajenga watoto  kuwa  na afya bora.
Nyambui  akifanya  mazoezi  na watoto kabla ya kuanza  kukimbia mbio za  kuishi.
Viongozi  na watoto  wakiwa katika picha  ya pamoja.
Watoto wakiigiza  jinsi  ukatili  kwa watoto  unavyotendeka ikiwa ni pamoja na wasichana kuolewa wakiwa katika  umri mdogo.
Kamati yaulinzi na usalama ya mkoa wa  Shinyanga.
Mkuu wa  mkoa wa Shinyanga Ally  Rufunga  akiwa  na  mwakilishi wa mkurugenzi wa nchi  ya Tanzania  wa  Shirika  la kimataifa  la kuhudumia  watoto .
Maandalizi  kabla ya kuanza mashindano  ya mbio  za  kuishi.
Wafanyakazi wa shirika  la Save  the  children Shinyanga  wakiwa  katika  picha ya pamoja  na viongozi.
Mashindano  ya  kukimbia mbio  za  kuishi yakiendelea.













No comments:

Post a Comment