Friday, October 31, 2014

YALIYOJIRI MGODI WA BUZWAGI ZIARA YA KAMATI YA BUNGE ARDHI MALIASILI NA MAZINGIRA YAWEKWA WAZI.

Mwenyekiti wa kamati  ya bunge ardhi  maliasili  na mazingira James Lembeli wa  pili kutoka kulia  ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kahama mkoani Shinyanga , akiwa  na wajumbe wengine wa kamati  hiyo pamoja na viongozi wa mgodi wa Buzwagi wakitoka  kukagua bwawa la kuhifadhia  maji
ambayo yametumika   kuoshea  dhahabu, ambapo kamati  hiyo ilijionea jinsi  mgodi  unavyotekeleza sheria ya kuhifadhi  mazingira migodini na  kupongeza  hatua hiyo kuwa migodi  mingine inatakiwa kuiga mfano  huo  kwani inasaidia kulinda afya za wafanyakazi  na wananchi  kwa  ujumla.
Wajumbe  wa kamati  ya bunge ardhi maliasili na mazingira wakiwa katika ukumbi uliopo ndani ya mgodi wa Buzwagi mara baada ya kutembelea kujionea  hali  halisi  ya utunzaji wa mazingira.
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa  mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na kampuni ya African barrick gold mine  uliopo wilayani  Kahama mkoani  Shinyanga.
Baadhi ya wajumbe wa kamati wakicheza ngoma ya  waswezi ambayo  ni maarufu katika mikoa ya kanda yaziwa ,aliyejitupia mtandio  mwekundu ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais mazingira Ummy  Mwalimu na aliyevaa suti  nyeusi ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ardhi maliasili na mazingira  James  Lembeli.
Waandishi wa habari  wakiwa kazini ni katika  mgodi wa Buzwagi
Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais  mazingira Ummy  Mwalimu aliyekaa kati kati akizungumza mara  baada ya kamati  hiyo kupokea taarifa iliyotolewa na meneja mkuu wa  mgodi wa  Buzwagi  Philibert Rweyemamu, ambapo aliwapongeza kwa kuwa na utaratibu  mzuri wa utunzaji wa mazingira mgodini na kuwataka kuongeza bidii  zaidi .
Naibu waziri akiwa na wajumbe wa kamati wakieleka kukagua bwawa la kuhifadhia  maji katika  mgodi huo.
Burudani ya  ngoma inaendelea








No comments:

Post a Comment