Shinyanga.
JESHI la polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia mwanamke
mmoja anayejulikana kwa jina la Pili Michael(24) kwa tuhuma za kusababisha
mauaji ya Stephen Philibert (30), baada ya kuvunja dirisha na kuingia ndani kwa
mwanamke huyo na kutaka kumbaka, ndipo
alipojihami kwa kumchoma na kisu kichwani.\
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tisa usiku mtaa wa
ngokolo manispaa ya Shinyanga wakati wakristu wakiendelea kusherehekea
sikuku ya pasaka,ambapo kijana huyo ambaye hivi sasa ni marehemu alikwenda
nyumbani kwa pili kisha kuvunja dirisha na kuingia ndani.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa
Shinyanga Evarist Mangalla ,alisema
kijana huyo aliyeuawa ni mkazi wa Ngokolo , alichomwa kisu kichwani wakati
akitaka kumbaka Pili Michael ndipo alijihami kwa kumchoma na kisu kichwani hali
iliyopelekea kupiga kelele za kuomba msaada.\
“Maelezo yaliyotolewa na mtuhumiwa ni kwamba Stephen
alivunja dirisha la nyumba ya mwanamke huyo anayeishi Ngokolo mjini Shinyanga
na kuingia ndani, katika harakati za kutaka kumbaka Pili kujihami kwake
alijihami kwa kumchoma kisu kichwani”,alisema kamanda Mangalla.
Kamanda Mangalla aliongeza kuwa mwanamme huyo baada ya
kuchomwa kisu kichwani alipiga kelele za kuomba msaada na kwamba watu
walikusanyika na kumpeleka hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu
lakini alifariki dunia akiwa katika hospitali hiyo.
Kaimu mganga mfawidhi
wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel ,alisema hospitali hiyo
haina taarifa kuhusu mwanamume huyo aliyeuawa kwa kuchomwa kisu kufikishwa
hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment