Friday, August 8, 2014

MGANGA WA KIENYEJI AUWA MGONJWA WAKE KWA KIPIGO ALIKWENDA KUTIBIWA

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya matukio mbalimbali ambayo yametokea mkoani Shinyanga.


MGANGA wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Mihayo Isheli  anatafutwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga baada ya kusababisha mauaji ya kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Vicent Kawawa(28),aliyekuwa anamtibu ugonjwa wa akili kwa kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kutoroka yeye na familia yake.

Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 12 jioni nyumbani kwa mganga huyo  katika kijiji cha Buduba kata ya Nyandekwa wilayani Kahama mkoa wa Shinyanya,baada ya mgonjwa aliyekuwa anatibiwa kichaa kupanda na kuanza kumpiga mganga wa jadi na watu waliokuwa kwenye mji huo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alimtaja kijana aliyeuawa kuwa ni Vicent Kawawa(28) ambaye anadaiwa kuwa na ugonjwa wa akili aliuawa na mganga wa kienyeji na watu waliokuwepo eneo la tukio.

Haya mauaji chanzo chake ni kwamba mgonjwa alipandisha kichaa na kuanza kumpiga mganga na watu waliokuwa eneo hilo, ndipo katika kumtuliza mganga alianza kumpiga akisaidiwa na watu hao ambao idadi yao haijajulikani na kusababisha kifo chake papo hapo”alisema kamanda.

Kamanda Kamugisha alisema baada ya tukio hilo mganga Mihayo Isheli alikimbia na familia yake  pamoja na watu waliokuwa katika eneo hilo,jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi sanjari na kumtafuta mganga huyo  na wahusika wengine waliokuwa katika eneo la tukio.

Na Stella Blog.

No comments:

Post a Comment