Kushoto ni mshindi
wa kwanza katika
mbio za kilomita 220 kutoka Shinyanga kwenda Kahama na kurudi Shinyanga
Goleha Ngusa kutoka kutoka Simiyu ambaye ameondoka na kitita
cha shilingi milioni moja,kulia kwake ni mshindi wa pili Daudi Helemala
kutoka Mwanza,ambaye
ameondoka na shilingi laki 8.
Mashindano
ya mbio za baiskeli kwa kanda ya ziwa na mashariki yamefanyika katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika leo
katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga yakiwa yamedhaminiwa na TBL
kupitia bia yake yake ya Safari Lager huku mgeni rasmi akiwa ni kaimu katibu
tawala msaidizi utawala na utumishi bwana Raymond Kiwesa kwa niaba ya mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.
Michezo ya
mbio za baiskeli iliyofanyika ni mbio za masafa marefu kwa wanaumme kilomita 220
kutoka Shinyanga kwenda Kahama na kurudi Shinyanga,mbio kwa akina mama kilomita
150 kutoka Shinyanga hadi Isaka na kurudi Shinyanga,mbio za watu wenye ulemavu
kilomita 12(kuzunguka uwanja wa kambarage mara 30),mbio za akina mama
wakiendesha baiskeli wakiwa wamebeba ndoo kichwani,ngoma za asili pamoja na
show mbalimbali.
Akitangaza
washindi katika mbio hizo za baiskeli,katibu wa chama cha baiskeli kanda ya
ziwa mashariki John Elisha amesema mbio za baiskeli kwa upande wa wanaume
kilomita 220 wametumia masaa 6 na dakika 6 kutoka Shinyanga kwenda Kahama na
kurudi Shinyanga.
Amemtaja
mshindi wa kwanza katika mbio hizo kuwa ni Goleha Ngusa kutoka kutoka Simiyu
ambaye ameondoka na kitita cha shilingi milioni moja,mshindi wa pili Daudi
Helemala kutoka Mwanza,ambaye ameondoka na shilingi laki 8,mshindi wa tatu
Simon Mbaruku kutoka Simiyu,ambaye amjenyakulia shilindi laki 6,mshindi wa nne
ni Masunga Duba kutoka Mwanza ambaye amejinyakulia laki 5 na mshindi wa tano
Nchuki Samweli kutoka Shinyanga ambaye ameondoka na shilingi laki 3 huku
washindi wa 6 hadi 10,laki 1 kila mmoja,washindi wa 11 hadi 20 kila mmoja
shilingi elfu 50.
Kwa upande
wa mbio za baiskeli kwa akinamama kilomita 15o kutoka Shinyanga kwenda Isaka na
kurudi Shinyanga mshindi wa kwanza ni Martha Anthony kutoka Mwanza ambaye ameondoka
na shilingi laki 7,mshindi wa pili Salome Donald kutoka Shinyanga,ameondoka na
shilingi laki 5,wa tatu Laurencia Luzuba kutoka Mwanza aliyejinyakulia shilingi
laki 3,mshindi wa nne Elizabeth Donald kutoka Shinyanga alipata laki 2 na
mshindi wa 5 ni Elizabeth Clement kutoka Shinyanga ambaye ameondoka na shilingi
laki 1 na nusu huku mshindi wa 6 hadi 10 kila mmoja akiondoka na shilingi laki
1 na wa 11 akiondoka na shilingi elfu 50 kama kifuta jasho chake.
Katibu huyo
wa chama cha baiskeli kanda ya ziwa mashariki amemtaja mshindi wa kwanza kwa kwa
upande wa mbio za akinamama wanaoendesha baiskeli wakiwa na ndoo kichwani kuzunguka
uwanja wa Kambarage kuwa ni Makirikiri Joseph ambaye amejinyakulia shilingi
laki moja na nusu,mshindi wa pili Christina Giti ambaye amepata shilingi laki
1,mshindi wa tatu Joyce Bundala aliyejinyakulia shilingi elfu 80,mshindi wa nne
Tatu Hassan aliyepata shilingi elfu 60,wa nne Jenny Shaban aliyeondoka na
shilingi elfu 50 huku mshindi wa 6 hadi 12 akiondoka na shilingi elfu 30 kama
kifuta jasho chao wote kutoka Shinyanga.
Kwa upande
wa mbio za baiskeli kwa watu wenye ulemavu kuzunguka uwanja wa Kambarage mara
30,mshindi wa kwanza ni Makende Derema aliyejinyakulia shilingi laki 1 na
nusu,mshinidi wa pili Ngalu Ngamba aliyondoka na shilingi laki 1,mshindi wa
tatu Peter Thomas aliyejinyakulia shilingi elfu 80,mshindi wa 4 Gogadi Shija
aliyeondoka na shilingi elfu 60 na mshindi wa 5 Shija Nkwabi aliyeondoka na
shilingi elfu 50.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi wote mgeni rasmi kaimu katibu
tawala msaidizi utawala na utumishi bwana Raymond Kiwesa kwa niaba ya mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ameipongeza kampuni ya bia bia ya TBL
kwa kuwa mstari wa mbele katika kudhamini mashindano hayo na kuwaomba waendelee
kusaidia sekta ya michezo pamoja na kwamba kila mara wamekuwa wakidhamini
michezo ya aina mbalimbali kama vile mpira wa miguu,pool table.
Kwa upande
wake meneja mauzo na usambazaji TBL kanda ya ziwa bwana Malack Sitaki amesema
miongoni mwa malengo ya TBL kudhamini
mbio hizo za baiskeli ni kuhamasisha michezo nchini,kuwa karibu na wateja wake
wa bia ya Safari Lager kutoa burudani kwa wananchi ukiangalia wananchi wengi
mkoani Shinyanga na kanda ya ziwa kwa ujumla wanapenda mbio za baiskeli.
Huu ni mwaka wa 16 tangu TBL
kupitia bia yake ya Safari Lager na mwaka huu washiriki walikuwa wanatoka mikoa
ya Geita, Kagera, Mara, Mwanza, Tabora, Shinyanga na Simiyu.
Na Malunde1 blog.
|
No comments:
Post a Comment