
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Butiama Anjelina Mabula aliyezungumza na TBC muda mfupi uliopita ajali hiyo amesema ajali hiyo imehusisha basi la AM Coach lenye namba za usajili T736 AWJ likitoka Musoma kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi T677 CYC J4 Express likitoka Mwanza kwenda Tarime na gari jingine dogo aina ya Nissan Corola P332 KKT
likitoka eneo la Sabasaba yote yalikutana kwenye mteremko yakitokea juu kwenda Darajani katika kupishana hawakuweza kupishana yakagongana na wakati huo gari dogo likapaki pembeni nalo likagongwa kwa nyuma likasukumwa na kutumbukia mtoni.
Katika gari dogo kulikuwa na watu 8,wawili wamefariki dunia na majeruhi 36 kutoka kwenye mabasi nao wamefariki na majeruhi 80 wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mara.
Madereva wote wamefariki dunia,na kwamba mizigo ya majeruhi iko chini ya ulinzi wa polisi
No comments:
Post a Comment