Wednesday, September 24, 2014

UGONJWA WA EBOLA BADO NI TISHIO:SERIKALI SASA YATAFAKARI WATU KUSALI NYUMBANI KUZUIA KUENEA ZAIDI

Serikali imesema ikiwa juhudi za kupambana na Ebola zitashuka, madhara yatakuwa makubwa zaidi
Rais wa Sierra Leone amesema kuwa serikali inatafakari kutangaza awamu ya pili ya amri ya kutotoka nje kote nchini ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa hatari wa Ebola.
Rais Ernest Bai Koroma, amesema kuwa kwa sasa ameridhika na mafanikio yaliyotokana na kuwazuia watu kutoka nje kwa saa 72 .
Awamu ya kwanza ya amri hiyo ilimalizika Jumapili.
Alisema kuwa maafisa wakuu walizuru zaidi ya nyumba milioni moja na kuwapata watu wengi ambao walikuwa wameathiriwa na ugonjwa huo.
Pia walipata mili ya watu waliokuwa wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Shirika la afya duniani limesema kuwa hadi pale hatua zaidi zitakapochukuliwa kukabiliana na janga la Ebola, visa vya maambukizi huenda vikaongezeka.

No comments:

Post a Comment