JESHI la
polisi mkoani Tanga,limenasa mtandao haramu wa usafirishaji na kufanikiwa
kuwakomboa watoto 13,waliokuwa wakisafirishwa kuelekea nchi jirani ya Kenya.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Tanga,SACP Frasser Kashai ametoa taarifa za tukio hilo jana
akisema kuwa watuhumiwa wa usafirishaji wa watoto hao wanashikiliwa na polisi
kwa hatua zaidi za kisheria na mahojiano.
Kamanda
Kashai alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 12,mwaka huu saa 17.30 jioni
huko wilayani Mkinga mkoani hapo eneo la Horohoro mpakani na nchi jirani ya
Kenya.
Kashai
aliwataja watoto waliookolewa ni Zalika Abeid (16)Bisura Husein (16)Mwanaid
Husein (18) wote wa kijiji cha Ntamwe wilayani Lushoto na Asimaya Sekanyorota
(20)Ashiruna Sekanyorota (20) ambao ni familia moja wa Wanga Lushoto na Seleman Ibrahim (20) wa Maligwe Lushoto.
Wengine ni
Rajabu Mohamed(15) wa Kwamnele Handeni,Mgaza Twaha (15) wa Mtamwe Lushoto,Mussa
Ayubu (17) wa Mlole Lushoto Abdully Hassani (17) mkazi wa Mlole wilayani Lushoto
mkoani hapo.
Pia wamo
Ally Adam (16) wa Kwamnele Handeni,Said Husein (22)wa kijiji cha Wangwe Lushoto
na Idd Rajabu wa mkazi wa Baga wilayani Lushoto.
Kwa mujibu
wa kamanda Kashai ni kwamba wanaoshikiliwa na polisi ni dereva wa gari
lililokuwa likisafirisha watoto hao SaLUM Hassan(39) na Hassan Salim (39) mkazi
wa Lushoto aliyekuwa muangalizi wa watoto hao na kwamba sasa unafanyika
utaratibu wa kuwapata wazazi wa watoto ili kurejeshwa makwao.
Taarifa za
awali zinaeleza kuwa watoto hao walikuwa wakipelekwa kwenye chuo cha kiislamu
kiitwacho Ummukuluthummu Muslim School huko Mombasa ambapo hata hivyo taratibu
za kisheria kwa usafiri wan je ya nchi hazikufuatwa.
Kamanda
Kashai aliongeza kwa kusema kwamba watoto hao walikuwa wakisafirishwa kwa gari
lenye nambari T702 CRZ Toyota Hiace huku ukaguzi ulipofanyika kwenye hati za
kusafiria iligundulika kuwa haukutiamia kutokana na kukosekana kwa barua za
ridhaa kutoka kwa wazazi wao.
Kutokana na
tukio hilo kamanda Kashai amewataka wananchi kufuata taratibu za kisheria kwa
kuwasiliana na idara ya Uhamiaji pindi wanapotaka kusafiri kwenda nje ya nchi
ambayo itasaidia kuepuka uwezekano wa kujitokeza kwa vitendo vilivyo kinyume na
taratibu za kisheria kwa kuzingatia misingi ya haki.
No comments:
Post a Comment